Thursday, February 9, 2012

Tanzania Electronic and Postal Communication Act 2009

Electronic and Postal Communication Act 2009 kwa lugha ya kigeni. Sheria hii imetungwa kwa lengo la kuhakiksisha sheria inatambua maendeleo mapya yaliyopo na yanayoendelea kujitokeza katika sekta ya mawasiliano ya kielektoniki.
Kwa kutambua hivyo sheria Ya Mawasiliano ya mwaka 1993 imefutwa na sheria hii mpya ya mwaka 2009.
Sheria mpya inatoa mamlaka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania au kwa lugha ya kigeni Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) kuhusu masuala mbalimbali ya mawasiliano ikiwa pamoja na kutoa leseni na kutunga sheria ndogo ndogo (regulations) mbali mbali katika sekta ya mawasiliano.
Ingawaje sheria hii mpya ainisha makosa mbali mbali ya kisheria katika sekta ya mawasiliano, lakini makosa hayajawekwa kwa mapana zaidi na hakuna muunganiko wa wazi kati ya sheria hii mpya na sheria ya Makosa ya Jinai (Penal Code Cap 16). Kwa mantiki hiyo basi makosa ya jinai yanayohusu mawasiliano ya kielektroniki (Cyber crimes) hayajapambanuliwa kwa uwazi na hayajaainishwa kwa mapana zaidi.
Sheria hii mpya imeainisha mambo kadhaa ya kisheria ambayo  katika hali ya kawaida raia wema wengi wa Tanzania wanaotumia simu za viganjani/mkononi  hatuyajui. Lakini ukweli wa mambo ndio huo.
Sheria mpya ya Mawasiliano ya kielektroniki  na Posta (Electronic and Postal Communications) ya Mwaka 2009.  Sheria Na. 4 ya mwaka 2009. Sheria hii ina mambo kadhaa yanayoweza kudhaniwa ni utani au dhihaka lakini ni mambo ya kuzangatia. Ni budi kuzingatiwa maana sheria hiyo tayari imeshaanza kufanya kazi.

Sasa soma yafuatayo:
  1. Ni kosa kisheria kuuza SIM card bila kupata ruhusa ya kampuni inayotoa huduma  ya mawasiliano mfano Vodacom, Zain au Tigo, na n.k.  Kwa maelezo zaidi angalia kifungu namba 127 cha Sheria hiyo
  2. Ni kosa kisheria  kumiliki simu ya mkononi /SIM card bila kithibitisho. Kifungu cha 128
  3. Ni kosa kisheria kumiliki simu ya mkononi/SIM card ambayo unashindwa kuthibitisha uhalali wa jinsi ulivyoipata au bila kuwa na uhakika au imani ya kuaminika kuwa umeipata kiuhalali .  Kifungu cha 129
  4. Ni kosa kisheria   kushindwa kuripoti upotevu au kuibwa/kuibiwa  simu au SIM card. Kifungu cha  130.
  5. Ni kosa kisheria kuharibu/kurekebisha uhalisia wa simu ya mkononi/SIM card. Kifungu cha 131
  6. Ni  kosa kisheria   kutumia simu ya mkononi/SIM card isiyosajiliwa. Kifungu cha 133
Haya na mengineyo mengi yanapatikana katika sheria tajwa hapo juu.

No comments:

Post a Comment